Sarkozy na Hollande wazomeana

Wagombea katika uchaguzi wa urais nchini Ufaransa wameshutumiana kwa udangayifu , katika kipindi pekee cha mjadala wa televisheni kabla ya kufanyika kwa duru ya pili ya uchaguzi wa urais siku ya jumapili.

Rais Nicolas Sarkozy amesema amekuwa akionewa kwa kulaumiwa kutokana na matatizo ya Ufaransa.

Katika wakati mmoja Sarkozy alimtaja mpinzani wake wa chama cha Kisoshalisti, Francois Hallande, kama mtu mwenye kuharibia watu sifa.

Bwana Hollande, amesema kuwa kama atachaguliwa atakuwa rais anayejali maslahi ya kiuchumi na kijamii.