Madaktari wafukuzwa kazi Lagos

Mamia ya madaktari katika mji mkuu wa kiuchumi nchini Nigeria, Lagos, wamefukuzwa kazi katika uamuzi uliochukuliwa na gavana wa jimbo hilo. Uamuzi huo ulifikiwa baada ya madaktari hao kugoma kufuatia mzozo wa mishahara.

Madaktari hao wanasema wenzao zaidi ya 1000 wamefukuzwa kazi, lakini serikali inasema ni madaktari 800 pekee ndio waliofutwa kazi.

Wauguzi wametumwa kushikilia hatamu katika hosipitali zote katika mji wa Lagos wakati wa mgomo huo. Wagonjwa kadhaa wameripotiwa kufariki dunia baada ya kukosa kuhudumiwa.

Mwandishi wa BBC anasema ni mara ya kwanza kwa afisa wa serikali kuchukua hatua kali kama hiyo.