Tymoshenko kutibiwa na kuanza kula

Idara ya magereza nchini Ukraine imesema kuwa kiongozi wa upinzani aliyefungwa jela, Yulia Tymoshenko,amepelekwa hosipitalini katika mji wa Kharkiv.

Bi Tymoshenko, ambaye alifungwa jela mwaka uliopita kwa madai ya kutumia vibaya madaraka wakati akihudumu kama waziri mkuu amekuwa akisusia kula akilalamika kuwa alipigwa akiwa jela.

Kiongozi huyo wa upinzani sasa amesema atamaliza mgomo wake wa kususia chakula .

Bi Tyomoshenko anahitaji kufanyiwa matibabu kwa mgongo wake, na atakuwa chini ya usimamizi wa daktari kutoka Ujerumani, baada ya maafisa wa Ukraine kumpiga marufuku kusafiri nje ya nchi.