sudan kusini yaondoa polisi wake Abyei

Abyeyi Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Eneo la Abyeyi linalozozaniwa na Sudan na Sudan kusini

Umoja wa Mataifa unasema kuwa Sudan kusini imeondoa kikosi chake cha polisi katika eneo la mpaka linalozozaniwa la Abyei.

Nchi za Sudan kusini na Sudan kila upande unadai eneo hilo dogo la mpakani lenye utajiri wa mafuta ni mali yake.

Msemaji wa Umoja wa mataifa Martin Nesi-rky amesema takriban polisi mia saba wa Sudan kusini waliokuwa kwenye eneo hilo wamehamishiwa maeneo mengine ya nchi hiyo.

Hata hivyo amesema itachukua siku kadhaa kudhibitisha ikiwa polisi wote wameondoka katika eneo hilo.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limetishia kuziwekea vikwazo nchi zote mbili, ikiwa hazitarejea kwenye mazungumzo ya amani ifikapo tarehe 16 mwezi huu wa Mei.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limetishia kuziwekea vikwazo nchi zote mbili, ikiwa hazitarejea kwenye mazungumzo ya amani ifikapo tarehe