AU kutafuta kiongozi mpya

Viongozi kadhaa wa Afrika wanakutana nchini Benin kutafuta njia ya kumaliza suintofahamu kuhusu uwongozi wa Muungano wa Afrika.

Mkutano wa Afrika mapema mwaka huu ulishindwa kuafikia uwongozi mpya katika tume ya AU. Viongozi wa nchi walishindwa kuamua kati ya kiongozi wa sasa Jean Ping na Waziri wa zamani wa mambo ya nje Afrika Kusini Nkosazana Dlamini-Zuma.