ICC yamsaka Kamanda wa FDLR

Mwendesha mashtaka Mkuu katika mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC Luis Moreno Ocampo, amsisitiza kutekelezwa kibali cha kuwakamata makanda wawili wa makundi ya waasi Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemkorasia ya Congo.

Miongoni mwao ni panoja na Jenerali muasi Congo anayekabiliwa na uhalifu wa kivita.

Kibali cha kumkatama Sylvestre Mudacumura Kiongozi wa kundi la waasi wa Ki-Hutu FDLR {Democratic Forces for the Liberation of Rwanda). Wawili hao wametuhumiwa kwa mauaji na ubakaji wa raia Mashariki mwa DRC.