Wahukumiwa kifo Somaliland

Mahakama moja ya kijeshi katika eneo la Hargeysa, huko Somaliland, imewahukumu kifo watu 17 baada ya kupatikana na hatia ya kuchochea machafuko na mapigano katika mji wa Hargeysa

Katika kisa hicho watu saba wakiwemo wanajeshi wanne waliuwawa.

Washukiwa hao walisema kuwa kambi hiyo ya jeshi ilikuwa imejengwa kwenye ardhi ambayo walimiliki kwa miaka mingi.

Somaliland kwa mara nyingi inaonekana kama eneo lisilo thabiti na hufanya uchaguzi mara kwa mara licha ya mzozo unaokumba nchi ya Somalia.