Dhuluma za kinyumbani ni janga kubwa

Shirika moja la Marekani limetoa wito kwa jamii ya kimataifa kutambua dhuluma ya kinyumbani kama janga la kibinadamu kote duniani.

Shirika hilo la International Rescue Committee linasema kwamba jambo hilo kwa mara nyingi limekuwa likipuuzwa na kutambuliwa kama tatizo la kinyumbani tu.

Shirika hilo linasema wanawake wengi wanaopigwa hushindwa kutekeleza kazi yao kama inavyopaswa kuwa na kwa hivyo kurudisha maendeleo nyuma.

Kundi hilo linasema kwamba tabia ya wanawake kupigwa ovyo hutokea zaidi katika mataifa yanayotoka kwenye vita au mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, hasa Magharibi mwa Afrika.

Alisema kwa kuwa ubakaji hutumiwa kama silaha wakati wa vita imekuwa kawaida kwa wanajeshi wanaorejea kutoka vitani kuendelea na dhulumua hiyo dhidi ya wanawake walio karibu nao.