Dawa bandia zatishia vita vya Malaria

Utafiti mpya umeonyesha kuwa hatua muhimu zilizopigwa Katika vita dhidi ya ugonjwa wa malaria zinatishiwa na kuwepo kwa takriban thuluti moja ya dawa bandia za ugonjwa huo katika kanda ya kusini mashariki mwa asia na barani Afrika.

Aidha Utafiti huo unasema ingawa dawa bandia ni tishio kwa afya ya umma, dawa hafifu zinapunguza kinga dhidi ya magonjwa.

Unapendekeza mamlaka za mataifa hayo kupiga vita dawa bandia na kuhakikisha kuwa viwango bora vya utengenezaji dawa vinaafikiwa.

Ugonjwa wa malaria huuwa takriban watu laki sita na nusu kila mwaka katika mataifa ya Afrika.