Roketi ya mizigo yazinduliwa Marekani

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Roketi ya Space x

Kampuni moja ya marekani SpaceX imezindua roketi ya kwanza ya kibiashara itakayotumika kupeleka huduma na bidhaa kwa kituo cha kimataifa cha angani.

Roketi hiyo inayofahamika kama Falcon-nine iliondoka katika eneo la Cape Canavera jijini Florida baada ya jaribio la kwanza kugonga mwamba siku ya jumamosi.

Inatarajiwa kuchukua siku mbili kufika katika kituo cha angani.

Ndege za serikali ndizo zimekuwa zikitumiwa kusafirisha chakula na huduma katika kituo hicho lakini shirika la NASA linataka kutoa huduma hiyo kwa kampuni za marekani za kibinafsi.

Mwandishi wa BBC ameeleza kuwa serikali inatumai hatua hiyo itapunguza matumizi yake kwa mradi huo na badala yake pesa hizo kutumika kwa utafiti zaidi katika anga.