Hisa za Facebook zazua utata

Kumetokea utata mpya kuhusu hisa za Facebook katika masoko ya hisa wiki iliyopita baada ya wasiwasi kuzuka kutokana na mauzo ya hisa hizo wiki iliyopita na jinsi zilizouzwa.

Wasimamizi wa fedha wanachunguza iwapo kiongozi wa mpango Morgan Stanley, aliwadokeza baadhi tu ya wateja wake kuwa faida ya hisa za Facebook zilizotarajiwa zimeshushwa daraja.

Morgan Stanley amekanusha hilo na kusema kuwa uuzaji wa hisa hizo ulifuata kanuni sahihi.

Bei za hisa za kampuni hiyo ya mtandao wa kijamii imeshuka tangu mauzo yake kuzinduliwa rasmi kwa umma Ijumaa iliyopita.

Matatizo ya kiufundi katika siku ya kwanza ya mauzo hayo yalisababisha baadhi ya wawekezaji kupoteza fedha.