Mali:Kapteni Sanogo ndiye rais wa mpito

Nchini Mali wafuasi wa kioongozi wa mapinduzi, Kapteni Amadou Sanogo, wamemtaja kuwa rais wa mpito wa taifa hilo.

Msemaji wa Kapteni Sanogo amesema, kiongozi wao anatathmini suala hilo la anatarajiwa kutoa uamuzi wake baadaye hii leo.

Mwezi Machi mwaka huu, wanajeshi walimuondoa rais Amadou Toumani Toure, wakisema kuwa hawakufurahishwa jinsi ya vita dhidi ya watu wa kabila la Tuareg ilivyokuwa ikiendeshwa, kaskazini mwa nchi hiyo.

Muungano wa kiuchumi wa nchi za afrika mashariki ECOWAS umekuwa ukijaribu kurejesha utawala wa kisheria nchini humo na ilimtaja Dioncounda Traore kama rais wa mpito wa taifa hilo.

Lakini wapinzani wa Traore walivamia ofisi yake siku ya jumatatu na kumjeruhi.