Umeneja wa biashara wapungua tija Ulaya

Utafiti wa mameneja wa biashara umeonyesha kuwa kazi hiyo katika biashara za Ulaya imeshuka kwa mwaka wa tatu mfululizo mwezi Mei.

Utafiti huo unaofanywa kila mwezi na kampuni ya Markit, unaonyesha kuwa uchumi unaendela kushuka na kasi yake inaongezeka.

Nchini Ujerumani takwimu zinaonyesha kuwa mapato ya sekta ya uzalishaji yameshuka kwa kiwango cha haraka karibu miaka mitatu iliyopita.

Takwimu hizo zilitangazwa saa chache baada ya viongozi wa Muungano wa Ulaya kumaliza mazungumzoyaomjiniBrussels.

Kwa kiasi kikubwa yalikuwa namna ya kukuza uchumi na yalimalizika kwa ahadi kuwa kufanya kila linalowezekana Ugiriki isitoke katika ukanda wa euro, lakini kukiwa na mpango madhubuti wa kuifanya isiondoke.