Rais Baraza la Upinzani Syria ajiuzulu

Baraza la Kitaifa la Upinzani nchiniSyria(the SNC) limesema limekubali kujiuzulu kwa Rais wake Burhan Ghalioun, ambaye ameongoza vuguvugu hilo tangu lianze mwezi September mwaka jana.

Limesema Bw Ghalioun ataendelea kuliongoza Baraza hilo mpaka atakapopatikana mrithi wake.

Haijajulikana nani atakuwa kiongozi baada yake.

Bw Ghalioun alishachaguliwa mara tatu, na hivi karibuni mwezi huu lakini uongozi wake katika SNC umekuwa ukikosolewa na wanaharakati hasa wale walio ndani yaSyria.

Baraza hilo la SNC limekuwa likosolewa pia kwa kushindwa kupata ushawishi na kuungwa mkono na Jumuiya ya kimataifa katika harakati zake nchini Syria.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa idadi ya watu waliokufa ni zaidi ya watu 9,000 tangu ghasia hizo za kumpinga Rais Assad zianze mwez Machi 2011