Uchumi wa Uingereza waporomoka zaidi

Uchumi wa Uingereza umeshuka zaidi kwa 0.3% katika miezi mitatu ya mwanzo wa mwaka, kuliko awali ilivyofikiriwa, takwimu mpya zimeonyesha.

Mwezi uliopita ilikadiriwa kuwa Ofisi ya Twakimu (ONS) ilionyesha kuwa uchumi utashuka kwa 0.2%.

Kupitiwa upya kwa takwimu za uchumi kunatokana na kushuka kwa kiwango cha mapato yanayotokana na biashara ya ujenzi kuliko ilivyotarajiwa.

Kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu uliopita, uchumi umeyumba kati ya ukuaji na kushuka kwa uchumi.

Katika miezi mitatu ya mwisho, uchumi pia umeshuka ikimaanisha kuwa Uingereza inarudi katika mdororo wa uchumi.

Kuna wasiwasi kuwa uchumi wa Uingereza utashuka yena katika robo nyingine ya mwaka, gavana wa Benki yaEnglandMervyn King ameonya kuwa Jubilee ya Malkia inaweza kupunguza mapatao.