Tetemeko la Arthi Italia

Tetemeko la arthi limetokea Kaskazini mwa Italia na kuwaua takriban watu wanane huku wengine wengi wakiaminika kufunikwa na vifusi.

Idara ya Giolojia Marekani imesema tetemeko hilo lilitokea majira ya asubuhi katika eneo la Bologna ambapo watu sita walikufa katika tetemeko jingine la arthi siku tisa zilizopita.

Majengo kadhaa ya kale yaliharibiwa katika eneo la Mirandola, ambapo watu wawili walikufa.

Katika eneo la San Felice sul Panaro watu watatu walikufa baada ya kiwanda kimoja kuporomoka.

Picha za runinga zimeonyesha watu zaidi ya 7,000 ambao wamepiga kambi nje eneo moja kwa sasa wakiwa wanatumia mahema kama makaaz ya muda.