Mhudumu wa misaada achiwa huru Darfur

Mfanyikazi wa kutoa misaada na raia wa Uingereza ambaye alitekwa nyara katika eneo la Darfur Sudan ameachiwa huru.

Patrick Noonan anahudumia shirika la mpango wa chakula duniani WFP.

Haijabainika ni kundi lipi lililomteka nyara.

Shirika la WFP limepongeza kuachuwa huru kwa mfanyikazi wake na kuonya usalama mbaya katika eneo la Darfur unahatarisha shughuli za kibinadamu eneo hilo.

Jumla ya wafanyikazi 40 wa WFP wametekwa nyara eneo la Darfur tangu mwaka wa 2009.