Muuaji anayesakwa ni mcheza filamu

Polisi wa Canadia wanasema mwanamme anayeshukiwa kutuma vipande vya mwili wa binadamu katika afisi za chama cha kisiasa mji mkuu Ottawa huenda amekimbilia Marekani.

Msemaji wa polisi amesema maafisa wa usalama wamekuwa katika makaazi ya Rocco Magnotta. Mwaka 2009 wavuti unaoaminika kuwa wake ulichapisha njia mbalimbali za kumfanya mtu kutoweka.

Bw Magnotta, anayejitambulisha kama mcheza filamu za ngono na mpenzi wa jinsia zote ameorodheshwa miongoni mwa wahalifu wanaosakwa na kitengo cha polisi wa kimataifa- Interpol.

Kesi hiyo hiyo ilianza Jumanne wiki hii baada ya mguu wa binadamu kupatikana ukiwa umewekwa ndani ya sanduku nje ya makaazi ya Magnotta. Polisi wamesema wanafuata ushahidi kwenye kanda ya Video inayomuonyesha Magnotta akimkatakata mwanamme aliye uchi mwenye asili ya Asia.