Clinton "Urusi inachochea vita Syria"

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton ameonya Urusi kwamba sera yake nchini Syria inachangia kuwepo vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Akizungumza nchini Udachi, Bi Clinton alisema Rais Assad huenda akaisikia Urusi na ndio maana amekuwa akiitaka Urusi kuunga mkono hatua mbadala dhidi ya utawala wa Damascus.

Japo Urusi imeunga mkono mpango wa amani wa mjumbe wa kimataifa Koffi Annan, imepinga azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuilaani serikali ya Syria na kumtaka Rais Assad kuachia madaraka.