Sheria ya hatari kuondolewa Misri

Sheria ya hatari ambayo imekuwepo kwa miaka mingi nchini Misri inaondolewa.

Watawala wa kijeshi wamesema kwenye taarifa kwamba licha ya sheria hiyo kuondolewa, watahakikisha usalama wa nchi utaendelea kuimarishwa hadi pale Rais mpya atakapochukua hatamu za uwongozi.

Kumekuwa na hali ya suitofahamu ikiwa sheria hiyo ilistahili kuendelea lakini mbunge wa Misri ameambia BBC hatua hiyo sharti iidhinishwe na bunge.

Sheria hiyo imekuwepo kwa zaidi ya miongo mitatu ambapo Wizara ya ndani ina mamlaka ya kuwaweka korokoroni watu bila kuwafungulia mashtaka bila kuwepo na muda rasmi.