Gavana wa benki kuu apinga sheria

Gavana wa Benki Kuu Nigeria, Lamido Sanusi, amekosoa miswada miwili ya sheria inayowasilishwa mbele ya bunge na kusema inahujumu uhuru wa benki.

Akizungumza na shirika la habari la Reuters, bw Sanusi amesema ikiwa sheria hizo zitapita wabunge watapata mamlaka ya kuamua bejeti ya benki kuu pamoja na kuamua bodi yake.

Wadadisi wa kiuchumi wamesema bw Sanusi amesaidia kuleta mageuzi muhimu katika mfumo wa benki nchini Nigeria baada ya msukosuko wa kifedha mwaka 2008.