Maiti za wapalestina zarejea nyumbani

Rais wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, ameongoza ibada maalum kutoa heshima kwa raia wa Palestina waliouawa wakati wakishambulia Israel tangu mwaka wa 1975.

Israel imesema hatua ya kurejesha maiti za raia hao ni ishara ya kujenga imani na Palestina.

Takriban majeneza 80 yaliyofunikwa kwa bendera za Palestina yaliwekwa nje ya Ikulu ya Rais mjini Ramallah.

Maiti 12 zilipelekwa katika eneo linalodhibitiwa na kundi la Hamas la Gaza.

Kwa Wapalestina warehemu walioletwa ni mashahidi lakini Israel inawaona kama magaidi.