Jeshi ladhibitti uwanja wa Ndege Tripoli

Wanajeshi wa serikali ya Libya wamedhibiti uwanja cha ndege wa kimataifa wa mji mkuu, Tripoli, kufuatia mzozo wa siku nzima uliotatiza usafiri wa ndege.

Kundi la waasi kutoka magharibi mwa mji wa Tarhouna liliteka nyara uwanja huo hapo jana na kuitisha kuachiliwa kwa kamanda wao, linalodai alipotea kwa misingi isio eleweka katika mji huo mkuu.

Kisa hicho cha hivi punde kimeongeza hofu zaidi juu ya hali ya usalama nchini Lbya tangu maandamano yalio m'ngoa na kumuua Muammar Gaddafi mwaka uliopita.