Mashirika ya umma huru Syria

Umoja wa mataifa umesema kuwa serikali ya Syria imekubali kuyaachilia mashirika ya kutoa misaada kufanya kazi katika mikoa minne ambayo imeshuhudia mapigano makali zaidi.

Afisa mmoja wa Umoja huo amesema kuwa serikali ya Syria imekubali kwa maandishi kuwaachia wafanya kazi wa kutoa misaada pamoja na magari yenye vyakula na misaaada mingine kuingia mikoa ya Homs, Idlib, Deraa na Deir al-Zour.

Alisema kuwa utekelezaji wa hayo utakuwa mtihani mkubwa wa kuonyesha iwapo serikali ya Syria kweli ina nia nzuri.