Watu 21 wauawa Afghanistan

Shambulio la bomu mjini Kandahar Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Shambulio la bomu mjini Kandahar

Polisi mjini Kandahar Kusini mwa Afghanistan wamesema takriban watu 20 wameuawa na wengine 22 kujeruhiwa kufuatia shambulio la bomu la kujitoa mhanga.

Ripoti zinasema shambulio hilo lilitokea katika eneo moja ambalo hutumiwa na madereva ambao magari yao husafirisha bidhaa za wanajeshi wa muungano wa NATO.

Uchunguzi wa awali umebainisha kuwa bomu hilo lilikuwa limetegwa kwenye pikipiki.

Shambulio hilo limetokea takriban kilomita moja kutoka uwanja wa ndege wa Kandahar