Marekani yataka ulinzi uimarishwe Libya

Afisa mmoja wa ubalozi wa Marekani nchini Libya ameiambia BBC kuwa bomu lililotegwa kando mwa barabara lililipuka Jumanne usiku karibu na ofisi za ubalozi huo mjini Benghazi.

Afisa huyo anasema hakuna aliyejeruhiwa. Amesema Marekani imeshtumu shambulio hilo na imeomba serikali ya Libya kuimarisha ulinzi katika maeneo yao nchini humo.

Kuna wasiwasi nchini Libya kuhusu uwezo wa Baraza la Mpito linalotawala kuhakikisha usalama baada ya kumuondoa madarakani Kanali Gaddafi mwaka uliopita.