Ivory Coast yakana kuwasaidia waasi

Rais wa Liberia Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais wa Liberia

Serikali ya Liberia imekanusha madai kuwa ilishindwa kuwazuia wanajeshi wa waasi wanaopinga serikali ya Ivory Coast walioko Mashariki mwa nchi hiyo kuwasajili watoto kuwa wanajeshi wao na kuanzisha vita katika vijiji kadhaa nchini Ivory Coast.

Waziri wa mawasiliano wa liberia, Lewis Brown, ameiambia BBC kuwa Liberia haitaunga mkono vitendo ama makundi ambayo yanatishia kuzua mtafaruku katika mataifa jirani.

Shirika la Human Rights Watch limesema wanamgambo wanaoaminika kuwa raia wa Liberia na Ivory Coast wanawalenga wafuasi wa kiongozi wa Ivory Cost Alassanne Ouattara na kuwa takriban watu 40 wameuawa.

Wavamizi hao wanasemekana kumuungana mkono rais wa Ivory Coast aliyeondolewa madarakani Laurent Gbagbo, wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo zilizopelekea zaidi ya watu 1,000,000 kuhama makwao na wengine wapatao 3000 kuuawa.