Makundi ya Tuareg yakabiliana

Waasi wa Tuareg na wapiganaji wa kiisilamu wameripotiwa kukabiliana vikali kaskazini mwa Mali, wiki moja baada ya ushirikiano waliotangaza kuunda kusamabaratika.

Walioshuhudia wamesema makundi yote yametumia silaha kali kushambuliana katika mji wa Kidal.

Haijabainika ikiwa kulitokea maafa. Ijumaa ya wiki jana Kundi la Tuareg MNLA ambalo hufuata misingi isiyo ya kidini lilipinga pendekezo la wapiganaji wa kiisilamu kusimamia eneo la kaskazini kwa misingi ya sheria ya dini ya kiisilamu-Sharia.

Kaskazini mwa Nigeria inadhibitiwa na waasi tangu kutokea mapinduzi ya kijeshi nchini Mali hapo mwezi March.