Ghasia za kidini chini Burma

Walinzi wa mpakani nchini Bangaldesh wamewazuia watu kuvuka mpaka wakati wakikimbia machafuko kati ya Waisilamu na Wa- Buddha katika nchi jirani ya Burma.

Maafisa wanasema wamezuia mitumbwi sita iliyowabeba wasiliamu wengi wa jamii ya Rohingya na kuwarejesha nchini Burma.

Hali ya tahadhari imetangazwa katika jimbo la Rakhine ambako takriban watu 17 wameuawa huku mamia ya nyumba zikiteketezwa katika ghasia ambazo chanzo chake ni mwanmke wa kibudha kubakwa na kisha kuuawa.

Watu wa jamii ya Rohingya kutoka jimbo la Rakhine na ambao idadi yao ni ndogo hawatambuliki kama raia wa Burma au Bangladesh.