Afya ya Mubarak si nzuri

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani nchini Misri, ameambia BBC kuwa rais wa zamani Hosni Mubarak ana matatizo ya kupumua pamoja na pia anakabiliwa na shinikizo la damu.

Lakini amekanusha madai kuwa Mubarak ana tatizo la kupoteza fahamu.

Kumekuwa na ripoti za kutofautiana kuhusu hali halisi ya kiafya ya rais huyo wa zamani aliyeng'olewa mamlakani kwa mapinduzi ya kiraia.

Mubarak alifungwa maisha jela wiki jana kwa kuamuru mauaji ya waandamanaji. Familia yake Mubarak imekuwa ikishinikiza serikali imruhusu aondolewe jela na kupelekwa katika hospitali ya kijeshi