Watauwa wa Katoliki waonywa na Vatican

Makao Makuu ya Vatican yametangaza kwamba watauwa wa Kikatoliki nchini Marekani sharti watetee na kufuata mafundisho ya imani hiyo.

Taarifa hiyo imefuatia mkutano kati ya maafisa wakuu wa Vatican na viongozi wa Kongamano la watauwa Marekani.

Hapo mwezi Aprili Makao Makuu ya Vatican yalilaumu Kongamano hilo kwa kutetea sera kali za uhuru wa jinsia kinyume na sheria ya imani Katoliki.

Viongozi wa watauwa wamesema kikao cha leo kimekuwa cha wazi. Watauwa hao wamekuwa wakilaumu Vatican kwa kupinga huduma zao kusaidia usawa katika jamii.