Jeshi la Yemen latwaa miji ya kusini

Jeshi la serikali nchini Yemen limekomboa miji ya kusini iliyotwaaliwa na makundi ya wapiganaji yenye uhusiano na mtandao wa Al Qaeda hapo mwaka jana.

Wapiaganji hao waliondoka maeneo ya Zinjibar na Jaar ili kuepusha maafa ya raia.

Hii ni hatua muhimu kwa Rais Abd Rabbo Mansour Hadi aliyeamrisha kuanzishwa harakati kali dhidi ya makundi ya wapiganaji wakati alipotawazwa.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetishia kuweka vikwazo kwa upande wowote utakaoyumbisha mchakato wa mageuzi ya kisiasa nchini Yemen.