Aung San Su Kyi ziarani Ulaya

Mtetezi mkuu wa demokrasi nchini Burma, Aung San Suu Kyi, yuko Geneva, Uswizi katika hatua ya kwanza ya ziara yake kuzitembelea nchi za Ulaya katika kipindi cha miaka ishirini iliyopita.

Kwanza atazuru makao makuu ya Shirika la Kazi Duniani ambalo kwa muda mrefu lilikuwa likifanya kampeni za kupinga utumwa na watoto kufanyishwa kazi nchini Burma.

Miongoni mwa nchi nyingine atakazotembelea Bi Suu Kyi ni pamoja na Norway, ambako atapokea rasmi tuzo ya amani ya Nobel, ambayo hakuwahi kupokea tangu atangazwe mshindi wa tuzo hiyo.

Na Aung San Suu Kyi atakwenda Uingereza, ambako aliishi hadi alipoingia katika harakati za kupigania mageuzi ya kidemokrasia nchini Burma mwaka 1988.