Mtandao wa kuhifadhi bahari Australia

Australia imetangaza kuanzishwa kwa mtandao mkubwa kuliko yote duniani ya uhifadhi wa maeneo ya baharini, yenye eneo la kilomita za mraba milioni moja nukta saba kuzunguka pwani yake.

Hatua hiyo inalenga kuhifadhi na kulinda viumbe vya baharini na kuweka kikomo cha maeneo ya uchimbaji mafuta na gesi katika bahari ya nchi hiyo.

Hata hivyo kumekuwa na upinzani dhidi ya mpango huo kutoka kampuni za kuchimba mafuta na gesi pamoja na sekta ya uvuvi.

Hatua hiyo inakuja huku mataifa yakikutana katika mji wa Rio de Janeiro katika mkutano mkubwa wa Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo endelevu.