Kemikali zachafua maji Ukanda wa Gaza

Mashirika ya kutoa misaada katika ukanda wa Gaza yametahadharisha kuwa chanzo pekee cha maji ya kunywa katika ukanda huo kimechafuliwa na kemikali za mbolea za viwandani na kinyesi cha binadamu.

Mashirika hayo Save the Children na Medical Aid for Palestinians yamelaumu hali hiyo kuwa ni matokeo ya kukosekana kwa uwekezaji katika sekta ya maji na uharibifu unaotokana na vita.

Mashirika hayo yameongeza kuwa idadi ya watoto wanaougua magonjwa ya kuhara, imeongezeka mara dufu katika kipindi cha miaka mitano kutokana na athari za maji hayo.

Msemaji wa Save The Children, Osama Dano, ameiambia BBC kwamba tatizo hilo limesababishwa na vikwazo vya Israel dhidi ya Wapalestina katika ukanda wa Gaza.