Maziwa yaliyochanganywa Mercury China

Kampuni moja kubwa zaidi ya kuuza maziwa nchini Uchina, ijulikanayo kama Yili, imeanza kuitisha maziwa iliyokuwa inauzwa katika maduka yake mbalimbali nchini, baada ya kugunduliwa kuwa maziwa hayo yalikuwa yamechanganywa na madini mengi aina ya Mercury.

Hii ni mojawapo tu ya kashfa za vyakula vyenye sumu kupatikana nchini Uchina.Mercury huharibu ubongo na figo.

Kampuni ya Yili haijaeleza jinsi madini hayo yalivyochanganyikana na maziwa.

Miaka minne iliyopita maziwa yalipatikana yamechanganyika na kemikali ya melamine na kuwaua watoto sita na kuwafanya maelfu wengine kuwa wagonjwa.