Mashambulizi mpakani mwa Misri na Israel

Jeshi la Israil linasema kuwa linawasaka watu wenye silaha karibu na mpaka wake na Misri baada ya wapiganaji kuwashambulia wajenzi waliokuwa wakijenga ua linalotenganisha mataifa hayo mawili.

Washambuliaji hao walimwua mtu mmoja.

Jeshi linasema kuwa kulikuwepo na mlipuko na washambuliaji wawili wakapigwa risasi na kuawa.

Lakini Serikali ya Israil inasema inashuku kuwa wanne kati ya washambuliaji hao wangali nchini Israil.

Wakaazi wa eneo hilo wameshauriwa waendelea kukaa manyumbani mwao. Shule katika eneo hilo zimefungwa.