Madhara ya unene kupita kiasi

Kwa mara ya kwanza watafiti wamejumulisha ukubwa wa watu wote duniani na kubashiri madhara yanayotokana na unene na uzito wa wanadamu.

Wanasayansi kutoka London School of Hygiene and Tropical Medicine, wamesema kuwa ongezeko la uzito wa watu linaweza kuleta madhara sawa na yale yanayotokana na wanadamu wengine zaidi ya Bilioni moja kwenye sayari ya Dunia.

Watafiti wanasema ingawa ni asilimia sita pekee ya wanadamu walio duniani wanaishi Marekani Kaskazini lakini wao kwa pamoja huchukua kipimo cha thuluthi moja ya wanadamu wote walio duniani