Kamanda wa jeshi la Yemen auawa

Maafisa wa kimatibabu nchini Yemen wamedokeza kuwa kamanda wa jeshi nchini humo ameuawa na washambualiji wa kujitolea mhanga waliomlipulia bomu.

Jemedari Salem Ali Qatan aliuawa alipokuwa akielekea kazini katika mji wa Bandari wa Aden.

Jeshi la Yemen limekuwa likipambana na wapiganaji wanaoungwa mkono na kundi la kigaidi la Al qaida Kusini mwa nchi hiyo.

Hivi maajuzi jeshi hilo lilikomboa maeneo mawili yaliyokuwa yametekwa na wapiganaji hao.