China yatoa fedha kwa IMF

Uchina imetoa msaada zaidi wa dola bilioni 43 kwa shirika la fedha ulimwenguni IMF, ili kutoa misaada kwa nchi zinazokabiliwa na matatizo ya kiuchumi.

Mataifa mengine wanachama wa muungano wa BRICS YA Brazil Urussii, India na afrika kusini vile yamehaidi kutoka dola bilioni kumi kila mmoja.

Kundi hili limesema msaada huo utategemea kutekelezwa kwa mageuzi ambayo yataipa mataifa yanayostawi uwezo wa zaidi wa kupiga kura katika bodi ya IMF.