Maandamano Misri kupinga jeshi

Wafuasi wa chama cha Muslim Brotherhood nchini Misri wanapanga kufanya maandamano kote nchini humo kupinga hatua za baraza la utawala wa kijeshi kujipatia madaraka makubwa.

Baada ya kura nyingi kuhesabiwa katika uchaguzi wa urais nchini humo, mgombea wa kiti hicho kwa tiketi ya chama cha Muslim Brotherhood, Mohammed Mursi, anaelekea kunyakuwa ushindi japo kwa kura chache.

Matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa siku ya Alhamisi.

Baraza la kijeshi limesisitiza kujitolea kukabidhi madaraka kwa rais mpya atakayechaguliwa mwishoni mwa mwezi huu.