Msaniii mashuhuri wa kike auawa Pakistan

Mwimbaji wa kike maarufu amepigwa risasi na kuuawa Kaskazini Magharibi mwa Pakistan.

Ghazala Javed na baba yake waliuawa jana Jumatatu katika jimbo la Peshawar na watu wenye silaha waliokuwa kwenye pikipiki. Polisi wanasema mauaji hayo huenda yanahusiana na ugomvi wa kifamilia.

Binti Javed, ambaye alikuwa akiimba kwa lugha yake ya asili ya Pashto, alitoroka kutoka Swat hadi Peshawar, miaka mitatu iliyopita wakati jeshi lilipovamia eneo walikokuwa wakiishi likiwatimua Wapiganaji wa kiislamu.

Aliolewa na mfanyabiashara lakini baadaye wakatalikiana.