Wahamiaji haramu wafa maji Malawi

Polisi nchini malawi wanasema wahamiaji haramu hamsini wameaga dunia baada ya mashua walimokuwa wakisafiria kuzama kaskazini mwa nchi hiyo.

Shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia masuala ya wakimbizi UNHCR, limesema walioangamia ni raia wa Ethiopia.

Inaaminika kuwa saidi ya watu sitini walikuwa ndani ya mashua hiyo.

Mwandishi wa BBC nchini humo, anasema kwa sasa ni msimu wa baridi na hakuna dalili ya kupata manusura zaidi.

Meli hiyo ilizama katika ziwa Malawi siku ya jumatatu usiku, lakinin habari hizo zimeanza kutolewa kwa kuwa eneo hilo ni mbali na hakuna mawasiliano.

Wahamiaji wengi haramu kutoka mataifa ya pembe ya afrika huelekea nchini afrika kusini kupitia malawi.