Waziri wa zamani Misri afungwa jela

Waziri wa zamani wa Misri Sahem Fahmi amehukumiwa kifungo cha miaka kumi miaka kumi na tano gerezani kutokana na kuiuzia Israel gesi asili kwa bei ya chini sana.

Bwana Fahmi amepatikana na hatia ya ubadhirifu wa mali ya umma.

Mfanya-biashara aliyehusishwa kwenye kashfa hiyo Hussein Salem naye amepewa kifungo kama hicho, akiwa mwenyewe hayuko Mahakamani.

Waendesha mashitaka wamesema mauzo ya gesi kwa bei nafuu kwa nchi ya Isreal yaliofanywa na serikali ya zamani ya Hosni Mubarak kumeigharimu serikali faida ya mamilioni ya dola.