Uturuki yapeleka majeshi mpakani

Serikali ya Uturuki inaongeza majeshi yake katika mpaka wake na Syria.

Msafara wa magari ya kijeshi ,vikiwemo vifaru na silaha zingine umeokana ukielekea katika mji wa mpakani wa Yayladagi, Kusini mwa Uturuki .

Magari ya kijeshi pia yanapelekwa katika maeneo mengine ya mipakani.

Hatua hiyo imechukuliwa siku chache baada ya Syria kuiangusha ndege ya kijeshi ya Uturuki iliyokuwa ikipaa juu ya bahari ya Mediterranean.

Uturuki inasema ndege za Syria zimekiuuka sheria za anga za kimataifa mara mia moja mwaka huu.