Rais mpya wa Misri kuapishwa

Maelfu ya wafuasi wa rais wa misri, Mohamed Morsi, wamekusanyika katika medani ya Tahrir, kusikiliza hotuba yake, siku moja tu kabla ya kuapishwa kwake.

Morsi anatarajiwa kuapishwa kesho mbele ya mahakama ya kikatiba, licha ya chama chake cha muslim bortherhood kutaka bwana morsi kuapishwa mbele ya bunge la nchi hiyo, ambalo lina idadi kubwa wa wabunge wa kiislamu wenye siasa kali.

Lakini mahakama ya kikatiba nchini humo ilivunja bunge la nchi hiyo mapema mwezi huu.