Nestle haijazuia dhuluma kwa watoto

Kampuni kubwa zaidi ya kutengeneza vyakula, Nestle, imeshutumiwa kwa kutofanya uchunguzi wa kutosha, ili kuzuia ajira na dhuluma dhidi ya watoto katika harakati za azalishaji na uuzaji wa zao la kakao.

chama cha kimataifa cha usawa katika ajira ambacho kiliteuliwa na kampuni hiyo ya nestle, kufanya uchunguzi, kilifuata safari ya zao hilo la kakao kutoka mashambani nchini ivory coast, hadi kwa wauzaji wa kimataifa ambao huuza zao hilo kwa kampuni hiyo.

Shirika hilo limesema watu wengi hujeruhiwa kwa panga wakati wanapovuna zao hilo na kuwa watoto na watu wazima wanafanya kazi katika mazingira duni katika mashamba ya kakao.

Kampuni ya nestle Imesema ajira ya watoto inakiuka maadili ambayo kampuni hiyo inaunga mkono.