Burma yawaachilia wafungwa

Maafisa wa utawala nchini Burma wamewaachilia huru wafungwa arobaini na sita wakiwemo wafungwa 22 wa kisiasa.

Gazeti moja rasmi limesema kuwa wafungwa hao wanaachiliwa kwa misingi ya kibinadamu na pia kuhakikisha uthabiti wa nchi ya Burma sawa na kuhakikisha uwiano wa kitaifa.

Kiongozi wa upinzani wa Burma, Aung Sang Suu Kyi, ambaye amerejea tu kutoka ziara yake ya Ulaya, ameitaka serikali kuwaachilia wafungwa wengine miatatu na thelathini waliosalia na ambao amesema ni wafungwa wa kisiasa.

.