Wananchi wa China waandamana

Serikali ya Uchina imekubali kusitisha ujenzi wa kiwanda kimoja cha shaba nyekundu katika mji wa Shifang, kusini magharibi nchi hiyo kufuatia siku mbili za maandamano, dhidi ya athari ya kiwanda hicho kwa mazingira.

Maafisa wa serikali mjini humo wanasema raia waliandamana katika barabara za mji huo na kwamba maafisa kadhaa wa polisi na raia walijeruhiwa kwenye machafuko hayo.

Baraza la mji huo limesema litajadiliana na raia kuhusu wasi wasi wao lakini pia limeonya kuwa litatoa adhabu kali ikiwa raia hao hawatasitisha kile kilichotajwa kama vukiukaji wa sheria.