Upinzani kupinga matokeo Mexico

Mgombea wa chama cha mrengo wa kushoto katika uchaguzi wa urais nchini Mexico amesema uchaguzi huo ulikumbwa na dosari nyingi na huenda akapinga matokeo hayo ikiwa mpinzani wake atathibitishwa kuwa mshindi.

Huku zaidi ya asilimia hamsini ya kura zote zikiwa zimehesabiwa, Andres Manuel Lopez Obrador wa chama cha PRD , yuko asilimia sita nyuma ya Enrique Pena Nieto, wa chama kilichowahi kutawala Mexico kwa zaidi ya miongo miwili .

Bwana Lopez Obrador amesema atatumia mbinu zote za kisheria kutetea uchaguzi huo.